Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
WAFUGAJI NA WADAU WAMEENDELEA KUNUFAIKA NA TEKNOLOJIA ZA TALIRI KATIKA MAONESHO YA NANENANE 2026
10 Aug, 2026
WAFUGAJI NA WADAU WAMEENDELEA KUNUFAIKA NA TEKNOLOJIA ZA TALIRI KATIKA MAONESHO YA NANENANE 2026

Wafugaji, wanafunzi, watafiti na wadau mbalimbali wa sekta ya mifugo wameendelea kujitokeza kwa wingi kutembelea banda la Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nanenane) 2026 yaliyofanyika katika viwanja vya John Samwel Malecela jijini Dodoma, kwa lengo la kujifunza na kupata elimu kuhusu teknolojia za kisasa za ufugaji zinazochochea ongezeko la uzalishaji na tija.

Kupitia maonesho hayo, wataalamu wa TALIRI wameendelea kutoa elimu kuhusu mbegu bora za malisho, lishe ya mifugo, uboreshaji wa mifugo, udhibiti wa magonjwa, pamoja na teknolojia mbalimbali zilizofanyiwa utafiti na kuthibitishwa kuwa na manufaa kwa wafugaji.

Wageni waliotembelea banda hilo pia wamepata fursa ya kuuliza maswali na kupata ushauri wa kitaalamu unaokidhi mahitaji yao.