WAFUGAJI WAPATIWA ELIMU YA MALISHO BORA
21 Jul, 2025

Katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) wafugaji wameendelea kupatiwa elimu ya malisho bora ya mifugo ili kuongeza tija ya ufugaji.
Elimu hiyo imetolewa na wataalamu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) katika banda la taasisi hiyo lililopo ndani ya viwanja vya Mwl. J. K. Nyerere jijini Dar es salaam.
Maonesho hayo yanaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Fahari ya Tanzania”
#taliriutafitikwamaendeleo