Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
WAFUGAJI WAPATIWA ELIMU YA UPIMAJI WA MAZIWA
28 Oct, 2025
WAFUGAJI WAPATIWA ELIMU YA UPIMAJI WA MAZIWA

Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Fortunatha Luena akitoa elimu ya upimaji wa ubora wa maziwa kwa lengo la kuangalia viini lishe muhimu ikiwemo protini, mafuta, maji yaliyopo kwenye maziwa na vinginevyo, pamoja na kupima maziwa ili kuangalia mabaki ya madawa aliyopewa mnyama kama yapo kwenye maziwa ili kuhakikisha usalama kwa afya ya mnywaji.

Majibu ya vipimo hivyo huwawezesha wafugaji kuboresha mifugo yao.

Fortunatha ametoa elimu hiyo kwa wafugaji mbalimbali waliotembelea banda la TALIRI lililopo ndani ya viwanja vya Shule ya Sekondari ya Usagara Jijini Tanga yalipokuwa yakifanyika Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yakiwa sambamba na kaulimbiu isemayo “Tuungane Pamoja Kupata Chakula kwa Maisha Bora ya Baadae”

Pamoja na elimu hiyo wafugaji wamepata fursa ya kuzijua teknolojia bora za mifugo zilizozalishwa na taasisi hiyo.