TUPAZE SAUTI ILI TUOKOE PUNDA, MNYETI

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti amewataka wadau wote wanaosimamia haki na ustawi wa wanyama kukemea vikali vitendo vitakavyosababisha kutoweka kwa Punda ili wanyama hao waendelee kuwasaidia wananchi katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Mhe. Mnyeti ametoa rai hiyo Mei 17, 2024 alipokuwa akifunga maadhimisho ya siku ya Punda Afrika Mashariki ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Dodoma yakiwa na kauli mbiu isemayo “Mwaka wa Uhifadhi wa Jamii za Punda Afrika”yakitanguliwa na shughuli mbalimbali ikiwemo mijadala iliyolenga kuchukua hatua mbalimbali za kunusuru kutoweka kwa mnyama huyo.
“Punda wamekuwa wakifanya kazi kubwa na muhimu sana katika sekta za kiuchumi ambapo katika shughuli za usafiri hivi sasa wamekuwa wakitumika kubeba mizigo vikiwemo vifaa vya ujenzi na siku za hivi karibuni tumeshuhudia wakibeba madini katika migodi mbalimali nchini” Ameongeza Mhe. Mnyeti.