FAHAMU AINA ZA MALISHO AMBAZO ZIMEFANYIWA UTAFITI NA KUPENDEKEZWA KIKANDA, TALIRI.

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) mbali na tafiti mbalimbali za mifugo na uhaulishaji wa teknolojia za mifugo zinazofanywa na Taasisi hiyo pia inafanya Tafiti za malisho, na katika tafiti hizo imependekeza aina mbalimbali za malisho ya nyasi, mikunde, na miti malisho inayoweza kustahimili vizuri kutokana na hali ya kijiografia ya kanda husika.
1. Nyasi
TALIRI imependekeza nyasi aina ya ‘Cenchrus ciliaris’ kutumika na wafugaji wa kanda zote Nchini kwani zinauwezo wa kustahimili vizuri kwenye mazingira yeyote ya hali ya hewa.
2. Mikunde
*Kanda zenye baridi mikunde aina ya ‘Desmodium’ inaota vizuri.
*Kanda zenye joto mikunde aina ya ‘Alfalfa’ inaota vizuri.
*Kanda zenye ukame mikunde aina ya ‘Microptilium, Siratro na Clitoria ternatea’ kustahimili vizuri.