Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
JIWE LISHE KUONGEZA PROTINI, NGUVU NA MADINI KWA MIFUGO
05 Aug, 2024
JIWE LISHE KUONGEZA PROTINI, NGUVU NA MADINI KWA MIFUGO

Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Ndg. Jovith Kajuna ameeleza kuwa jiwe lishe la kulamba mifugo inayocheua lililozalishwa na taasisi hiyo lina viinilishe vinavyoongeza protini kwa wanyama kutokana na uwepo wa mashudu ya alizeti yaliyosagwa na majani ya miti malisho yaliyokaushwa na kusagwa, lakini pia kuna viini lishe vinavyosaidia kuongeza nguvu kwa wanyama kutokana na uwepo wa molasis na pumba za mahindi.

Kajuna ameeleza hayo leo tarehe 03/08/2024 alipokuwa akitoa elimu ya teknolojia za mifugo zilizoibuliwa na TALIRI kwa wadau mbalimbali wa mifugo waliotembelea banda la taasisi hiyo kwenye Maonesho ya 31 ya Kilimo ya Kimataifa ‘Nanenane’ ambayo kitaifa yanafanyika katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma yakiwa na kauli mbiu isemayo ‘Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi’

Sambamba na hayo Kajuna ameeleza kuwa kama ilivyo kwa mawe mengine ya madini ya kulamba mifugo, jiwe hili pia ni chanzo cha madini kwa mifugo.