FAHAMU NJIA RAHISI YA KUTENGENEZA HAY
21 Jul, 2025

Kwa mchungaji wa mifugo, hii ni fursa yako ya kujifunza jinsi ya kutengeneza nyasi kwa kutumia njia rahisi. Kwa kutumia sanduku maalum la mbao, unaweza kuandaa nyasi kwa urahisi na kuzihifadhi kwa ajili ya kulisha mifugo yako wakati wa kiangazi, wakati malisho ni machache.
Kufahamu zaidi juu ya ufugaji nyasi, tembelea hema la Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) lililopo ndani ya viwanja vya Mwalimu J. K. Nyerere jijini Dar es Salaam, kunakofanyika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba).
Pia, usisahau kufuata ukurasa huu kwa sasisho zaidi.