WAFUGAJI WAPATIWA BOKSI ZA KUTENGENEZEA ROBOTA ZA MALISHO
01 Apr, 2025

Mhe. Neale Richmond Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Ireland akigawa boksi za kutengenezea robota za malisho kwa wafugaji wa Wilaya ya Muheza wanaonufaika na Mradi wa Maziwa Faida ili kuwawezesha kuwa na uwezo wa kutunza malisho kwa ajili ya kipindi cha kiangazi ambapo kwa kutumia boksi hizo wafugaji wataweza kufunga robota kirahisi.
Zoezi hilo limefanyika leo tarehe 15/03/2025 katika ziara ya Waziri huyo alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Tanga kwa lengo la kujionea namna taasisi hiyo inatekeleza Mrari wa Maziwa Faida.