Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
WAFUGAJI HANDENI WAAHIDI KUCHANJA MIFUGO KWA WINGI
21 Jul, 2025
WAFUGAJI HANDENI WAAHIDI KUCHANJA MIFUGO KWA WINGI

Wafugaji Wilayani Handeni wameipokea Kampeni ya Chanjo ya Mifugo Kitaifa vizuri na kumuahidi Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujitokeza kwa wingi katika kuchanja Mifugo yao ili kutokomeza Magonjwa hayo ya Mifugo ili kuongeza tija kwenye Mifugo.

Akizungumza katika zoezi la Uhamasishaji na Utoaji Chanjo za Mifugo leo Julai 5, 2025 Wilayani Handeni Mkoani Tanga katika Kata ya Mazingara Kijiji cha Suwa, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mazingara, Bw. Rajabu Mwegole, amesema Mifugo inapochanjwa na kutambuliwa inaleta Usalama kwa Mifugo yenyewe na walaji.

“sisi kama Handeni tunashukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kututhamini wafugaji na kutuletea Kampeni hii ya Chanjo za Mifugo Kitaifa, na sisi wafugani tunamuhaidi kuanzia leo hii tunaanza kuchanja Mifugo yetu ili kutokomeza magonjwa ya mifugo na kuongeza tija katika Masoko ya nje ya nchi.” amesema Mhe. Mnzava

Aidha, Bw. Mwegole amewataka Wafugaji wote wa Handeni na Mkoa wa Tanga kiujumla, wajitokeze kwa wingi kuitumia fursa hii ya Mheshimiwa Rais ili kuweka kutokomeza vifo vya Mifugo, kwani bei za chanjo hizi ni sawa na bure kwani chanjo yang’ombe ni tsht. 500, Mbuzi/Kondoo tshs. 300 pamoja na kuku ambao wanachanjwa bure.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Prof. Erick Komba amesema kuwa Mifugo inakabiliwa na Changamoto nyingi ikiwemo changamoto ya maji, Malisho na Magonjwa, na Changamoto ya Magonjwa ndio imekuwa changamoto kubwa sana inayopelekea vifo vya Mifugo na soko la mifugo kuwa duni katika Masoko ya nje.

Vilevile, Prof. Komba amewapa salamu wafugaji kutoka kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji kuwa wafugaji waitumie fursa hii adhimu na waikimbilie, kwani chanjo hizi ni salama na zinazalishwa hapa hapa nchini na viwanda vya ndani.

#taliriutafitikwamaendeleo