Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
JOSHO LA KWANZA AFRIKA MASHARIKI, TALIRI MPWAPWA
12 Apr, 2025
JOSHO LA KWANZA AFRIKA MASHARIKI, TALIRI MPWAPWA

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kituo cha Mpwapwa inajivunia kuwa na historia ya uwepo wa Josho la kwanza Afrika Mashariki lenye miaka zaidi ya 100 lililojengwa na Wajerumani mwaka 1905.

Hayo yameelezwa na Bi. Marry Milinga Afisa Shamba Mwandamizi kutoka TALIRI Mpwapwa. Mary ameendelea kueleza kuwa josho hilo hadi sasa linatumika kuogeshea mifugo na hivyo kuepusha magonjwa yaenezwayo na kupe kwa mifugo ikiwemo ndigana.

“Kabla mifugo kuingia ndani ya Josho inapitishwa kunywa maji ili kuiepusha kutokunywa maji yaliyopo ndani ya josho ambayo yanamchanganyiko wa dawa za kuongeshea mifugo” ameeleza Mary.

Aidha, Mary ametoa wito kwa wafugaji kuogesha mifugo yao angalau mara moja kwa wiki ili kuiepusha na magonjwa.

Mara nyingi mifugo inayoogeshwa kwenye josho ni ng’ombe na mingine kama mbuzi huogeshwa kwa njia ya kupuliziwa dawa.