Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
DKT. OJANGO: MRADI WA TDGG UTAIMARISHA UBORESHAJI WA VINASABA VYA NG'OMBE WA MAZIWA KWA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA
25 Jun, 2026
DKT. OJANGO: MRADI WA TDGG UTAIMARISHA UBORESHAJI WA VINASABA VYA NG'OMBE WA MAZIWA KWA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA

Dkt. Julie Ojango, Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), akielezea utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Vinasaba vya Ng’ombe wa Maziwa katika Ukanda wa Kitropiki (TDGG), ambapo amesema kuwa mradi huo ni mpango wa kimataifa unaotekelezwa katika nchi mbalimbali kwa lengo la kusaidia serikali na sekta za maziwa kuanzisha na kuimarisha mifumo ya kitaifa ya uboreshaji wa ng’ombe wa maziwa inayotegemea matumizi ya takwimu, teknolojia za kidijitali, genomics na usimamizi bora wa mifugo, kwa lengo la kuongeza tija, faida na ushindani katika biashara ya maziwa.

Aidha, Dkt. Ojango amesema matarajio ya Mradi ni kuona nchi zote za ukanda wa kitropiki zinatumia fursa ya kuanzisha na kuendeleza mfumo wa TDGG, ambao unawezesha ukusanyaji, usimamizi na matumizi ya takwimu za mifugo kwa njia ya kidijitali, hatua itakayochangia kuboresha uzalishaji na maendeleo endelevu ya sekta ya maziwa.