DKT. MLAWA ATEMBELEA BANDA LA TALIRI

Watafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) wakiongozwa na Bw. Gilbert Msuta Meneja Sehemu ya Uhaulishaji wa Teknolojia (wa pili kulia) wakielezea aina za mbegu mbalimbali za malisho zilizofanyiwa utafiti na Taasisi hiyo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Angelo Mwilawa (wa kwanza kulia) alipotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya banda la Wizara hiyo wakati wa maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara ya yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam.
Maonesho hayo yanaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Tanzania: Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji”
Tembelea banda la TALIRI kujifunza teknolojia mbalimbali za mifugo zilizoibuliwa na Taasisi hiyo.