WANANCHI WAFAIDIKA NA ELIMU YA UBORA WA MAZIWA NA MALISHO KUPITIA TALIRI
22 Jun, 2026
Wananchi mbalimbali wamepatiwa elimu kuhusu masuala ya ufugaji, teknolojia za kisasa za mifugo na huduma zinazotolewa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), baada ya kutembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Viwanja vya Mbogo Ranchi wilayani Chalinze Mkoa wa Pwani yanapoendelea Maonesho ya Mifugo na Mnada wa Kimataifa.
Ambapo walipatiwa elimu juu umuhimu wa kupima ubora wa maziwa na elimu ya uzalishaji na utunzaji wa malisho ili kuongeza tija ya ufugaji na kuzingatia afya ya mlaji
TALIRI inaendelea kuhamasisha matumizi ya teknolojia na mbinu bora za ufugaji kwa maendeleo endelevu ya sekta ya mifugo nchini.
