Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
ZIARA YA MKURUGENZI WA PROGRAMU YA MIFUGO, TABIANCHI NA MAZINGIRA (LCE) ILRI
10 Aug, 2026
ZIARA YA MKURUGENZI WA PROGRAMU YA MIFUGO, TABIANCHI NA MAZINGIRA  (LCE)  ILRI

Wakati maonyesho ya kila mwaka ya kilimo ya Nanenane yakiendelea jijini Dodoma, tulipokea ziara ya kushtukiza kutoka kwa Dkt. Anthony Whitbread, ambaye ni Mkurugenzi wa Programu ya Mifugo, Tabianchi na Mazingira (LCE) katika taasisi ya ILRI(International Livestock Research Institute). Alitupongeza kwa kazi nzuri tunayofanya ya kuwaelimisha wakulima kuhusu umuhimu wa kutumia teknolojia rafiki katika ufugaji. Tunawakaribisha wote katika banda letu kwenye viwanja vya Nanenane jijini Dodoma, ambapo tutaonyesha umuhimu wa kuweka alama (tagging), kuzungushia uzio, na kupima uzito wa mifugo.