Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
kitabu cha mawasiliano ya wataalum wa mifugo chazinduliwa TALIRI TANGA
30 May, 2024
kitabu cha mawasiliano ya wataalum wa mifugo chazinduliwa TALIRI TANGA

Kitabu cha mawasiliano ya wataalamu wa mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Tanga Tanzania kimezinduliwa na Prof. Riziki Shemdoe Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika hafla ya uzinduzi wa miundombinu ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) ya kituo cha kanda ya Mashariki TALIRI Tanga iliyojengwa kupitia mradi wa maziwa faida.

Kitabu hicho kimeandaliwa na Mkurugenzi wa TALIRI Kanda ya Mashariki Dkt. Zabroni Nziku kupitia mradi wa maziwa faida kwa lengo la kuwawezesha wafugaji wa Tanga Wilaya ya Muheza kupata mawasiliano sahihi ya wataalamu wa kwenye maeneo yao ili kuweza kutatua kwa urahisi changamoto zinazoweza kuwakabili katika shughuli zao za ufugaji.

Aidha, vitabu 200 vimegaiwa kwa wafugaji, Afisa ugani, viongozi wa vyama vya ushirika wa ng’ombe wa maziwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza.

Kitabu hicho kitakuwa kinaboreshwa kila mwaka ilikukidhi mahitaji ya wakati huo.