Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
BONANZA LA WATUMISHI WA TALIRI MAKAO MAKUU
24 Feb, 2025
BONANZA LA WATUMISHI WA TALIRI MAKAO MAKUU

Leo tarehe 01/02/2025 Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Makao Makuu wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Prof. Erick Komba wamefanya bonanza lililojumuisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvuta kamba, kukimbiza kuku na riadha lengo ikiwa ni kuimarisha afya za watumishi hao kitendo ambacho kitachochea kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu.

Bonanza hilo litapelekea kuongeza ari ya ufanyaji mazoezi kwa watumishi hao ili kusaidia kuwa afya njema na hivyo kuwaepusha na magonjwa yasiyoambukiza kama presha, kisukari na mengineyo.