Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: TUKIO LA UTEKETEZAJI WA VIFARANGA KWENYE MPAKA WA NAMANGA ARUSHA
19 Dec, 2023 Pakua

Katika kipindi cha kuanzia tarehe 30.10.2017 kumekuwepo na taarifa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu kukamatwa na kuteketezwa vifaranga vya kuku 6,400 katika kituo cha ukaguzi wa mifugo na mazao yake cha Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la mji mdogo wa Namanga mkoani Arusha. Baada ya kukamata kwa shehena ya vifaranga hao na kubainika kwamba hawakuwa wameingizwa kwa kufuata taratibu za kisheria, Wizara kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya serikali vya ulinzi na usalama pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania waliviteketeza vifaranga hivyo kwa kuvichoma moto. Kitendo hicho kimezua mjadala katika mitandao ya kijamii kuhusu ya hatua zilizochukuliwa.