WATUMISHI TALIRI WAJENGEWA UWEZO JUU YA SHUGHULI ZA KITAFITI
01 Apr, 2025

Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo kwenye maeneo mbalimbali ya kitafiti lengo ikiwa ni kuongeza tija kwenye shughuli za utafiti.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha TALIRI Tanga yametolewa na Dkt. Egidius Kamanyi Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kufunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Prof. Erick Komba.