Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
HATUA ZA KUKAMUA NG'OMBE WA MAZIWA
29 Jul, 2024
HATUA ZA KUKAMUA NG'OMBE WA MAZIWA

1. Ng’ombe apumzishwe mara baada ya kutoka machungani.
2. Ng’ombe apelekwe sehemu maalumu iliyotengwa kwa ajili ya kukamulia maziwa.
3. Safisha kiwele (chuchu) za ng’ombe kwa maji ya vuguvugu.
4. Paka mafuta maalumu ya kukamulia kwenye chuchu za ng’ombe kwa ajili ya kuzuia chuchu kuchubuka.
5. Anza kukamua na hakikisha unamaliza maziwa kwenye chuchu zote.
6. Chuja maziwa na yahifadhi sehemu salama.