WAZIRI BASHIRU ATEMBELEA KITUO CHA TALIRI MPWAPWA
29 Oct, 2026
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, Wilayani Mpwapwa, alipotembelea na kukagua shughuli zinazotekelezwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI).
Katika Ziara hiyo iliyofanyika Oktoba 27, 2026 Mhe. Balozi Dkt. Bashiru alipokelewa na Mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mhe. Dkt. Sophia Kizigo, Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na wataalam kutoka wilayani na wa Taasisi za TALIRI na LITA.
