Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
Dkt Mwemezi Lutakyawa Kabululu
Mwemezi Lutakyawa Kabululu photo
Dkt Mwemezi Lutakyawa Kabululu
Mkurugenzi wa kanda ya kati

Barua pepe: mwemezi.kabulul@taliri.go.tz

Simu: 0757680338

Wasifu

Mwemezi Kabululu (BVM, MPhil., PhD)

Afisa Utafiti Mwandamizi

Barua pepe: mwemezi.kabululu@taliri.go.tz, mwemezie@gmail.com;

Simu (WhatsApp): +255 757 680 338

ORCID: 0000-0002-8621-9411

Web of Science Researcher ID: IYT-3333-2023

Dkt. Mwemezi Kabululu ni Daktari wa mifugo, Mtaalamu wa parasitolojia na Afya Moja, mwenye uzoefu wa miaka 15 katika utafiti wa afya ya mifugo na afya ya jamii. Alipata shahada yake ya uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mwaka 2020, akibobea katika parasitolojia na afya ya jamii ambapo utafiti wake ulilenga kutathmini afua za kudhibiti ugonjwa wa cysticercosis unaosababishwa na minyoo tegu ya nguruwe - Taenia solium.

Dkt. Kabululu alijiunga na TALIRI mwaka 2009 na kwa sasa ni Mkurugenzi wa Kanda ya Kati. Uzoefu wake wa kikazi unajumuisha nafasi mbalimbali, zikiwemo Daktari na Meneja wa Ranchi, utoaji huduma ya afya ya wanyama kwa wafugaji na utafiti wa magonjwa ya wanyama. Dkt. Kabululu ameongoza na kushiriki katika miradi kadhaa ya utafiti juu ya magonjwa, hasa yale yanayoambukizwa baina ya wanyama na binadamu, akijikita zaidi katika maambukizi ya Taenia solium kwa binadamu na nguruwe.

Dkt. Kabululu  amewasilisha mada katika mikutano na makongamano ishirini ya kisayansi na kitaaluma ya ndani na nje ya nchi, yakiwemo kongamano la dunia la Afya Moja (World One Health Congress) na kongamano la kimataifa la parasitolojia (International Congress of Parasitology – ICOPA). Mada yake aliyowasilisha katika Kongamano la saba la Dunia la Afya Moja lililofanyika nchini Singapore mwaka 2022 ilipata tuzo ya kuwa miongoni kwa mada bora zilizowasilishwa.

Dkt. Kabululu ameandika makala 24 zilizochapishwa kwenye majarida ya kisayansi yanayoheshimika, na pia ametumika kufanya mapitio (peer reviewer) kwa makala zinazowasillishwa katika majarida saba ya kisayansi.