WATAALAMU WA INTA, TALIRI WAKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA
26 Nov, 2024
Timu ya wataalamu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) wakiongozwa na Prof. Erick Komba Mkurugenzi wa taasisi hiyo (aliyevaa suti ya blue) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wataalamu kutoka Taasisi ya Kitaifa ya Teknolojia ya Kilimo ya Argentina maarufu kama INTA (Instituto Nacional de Tecnologia Agropecuaria) walipotembelea ofisi ya TALIRI kwa ajili ya majadiliano juu ya uanzishwaji wa mradi unaotarajiwa kutekelezwa na TALIRI wa kuboresha teknolojia za ufugaji katika maeneo kame na nusu kame.