Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
Ajenda za Utafiti

Agenda kuu ya Kitaifa ya Utafiti ni nyenzo muhimu inayotoa dira inayowaongoza

Watafiti katika kupanga na kutekeleza miradi ya kitafiti kwa kuzingatia mahitaji ya wadau

wa sekta ya mifugo. Agenda kuu ya kitaifa ya Utafiti ilitayarishwa kwa kushirikiana na wadau

mbalimbali ambapo walianisha vipaumbele muhimu saba (7) kama ifuatavyo:

  1. Uboreshaji Mbari za Mifugo
  2. Uboreshaji wa Malisho na vyakula vya Mifugo
  3. Uimarishaji wa Afya ya Mifugo
  4. Uimarishaji wa masuala ya Kiuchumi, kijamii na kitamaduni
  5. Utafiti katika Mifugo ilisiyozoeleka
  6. Utafiti wa masuala mtambuka, na
  7. Uongezewaji wa Thamani kwa mazao ya mifugo

Vipaumbele vilivyoainishwa kwenye agenda kuu ya kitaifa ya Utafiti wa Mifugo vimezingatia

matumizi sahihi wa teknolojia na bunifu mbalimbali ili kufikia malengo tarajiwa ya kuongeza tija

ya uzalishaji mifugo