Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
Wafugaji Kutoka Kiteto wametembelea TALIRI Makao Makuu kwa ajili ya Kujifunza Kilimo cha Malisho Bora
29 Feb, 2024
Wafugaji Kutoka Kiteto wametembelea TALIRI Makao Makuu kwa ajili ya Kujifunza Kilimo cha Malisho Bora

Wafugaji Kutoka Kiteto wametembelea TALIRI Makao Makuu kwa ajili ya Kujifunza Kilimo cha Malisho Bora

Wafugaji wawili kutoka Kijiji cha Ngurusero wiliya ya Kiteto wametembelea TALIRI Makao Makuu Kujifunza namna ya kuanzisha Kilimo cha malisho bora. 

Wafugaji hao ( Joseph Kakaa na Mollel Lemaseto) wamepokelewa na Mtafiti na mtalaamu wa malisho Bwn John Said Diyu na kupata elimu ya namna ya kuanzisha shamba la malisho bora aina ya Bufeli, Brachiaria, Juncao, Super Napier na Alfalfa. 

Wafugaji hao pia wametembelea vitalu vya utafiti wa malisho vilivyopo TALIRI Makao Makuu na kufurahia kuona malisho bora. 

Mtafiti Diyu aliwasisitiza kuwa ni lazima waboreshe mifugo yao kwa kununua madume bore ya ng'ombe kama Mpwapwa, Simmental, Brahman, Boran na Sahiwal kwa ajili ya kuongeza ubora wa ng'ombe wa nyama na kuongeza uzalishaji wa maziwa  na madume ya mbuzi bora aina ya malya kwa ajili ya kuboresha mbuzi wa asili. 

Wafugaji hao walishukuru sana kwa jinsi watafiti walivyowapa elimu muhimu na wameahidi kuwa mfano wa kuigwa kwa wafugaji wote waliya ya Kiteto na wanatarajia kupanda malisho ya kutosha kuweza kuzalisha mabunda ya hei (majani makavu) kwa ajili ya kuyahifadhi kwa matumizi ya mifugo yao na kuwauzia wafugaji wengine kipindi cha kiangazi ili kupunguza janga la mifugo kufa kwa kukosa malisho kipindi cha ukame wilayani Kiteto.